burundi bwacu

dimanche 13 octobre 2019

Mpya za Leo: MAGONJWA YA NGONO KWA VIJANA

Mpya za Leo: MAGONJWA YA NGONO KWA VIJANA: Kuna athari nyingi ambazo kijana anaweza kukumbana nazo kutokana na kuambukizwa magonjwa mbalimbali ya ngono. Magonjwa ya ngono yasipoti...

mardi 3 septembre 2019

samedi 29 juin 2019


Résultat de recherche d'images pour "université du burundi"
 Maisha ya Mwanachuo mjini Bujumbura

Katika nchi yetu ya Burundi, kama ilivyo katika nchi nyingine, kuna wingi wa vyuo. Ukitoa Chuo kikuu Cha Burundi na chuo kikuu cha Ualimu ENS ambavyo ni vya serikali, kuna pia vyua vyingi ambavyo ni vya watu binafsi. Na hivyo mtu hulipa ili aweze kupata masomo ya vyuo hivyo.
Kila mwaka, vyuo hivyo(vya kiserikali na visivyo vya kiserikali)huwaleta wanafunzi kutoka shule mbalimbali za sekondali nchini kote.Ndiyo maana ningependa niyazungumuzie kwa ufasaa maisha ya mwanachuo mjini Bujumbura.
Vyuo vinawapokea wanafunzi wengi.baadhi ya hao wanatoka vijijini mbali na mji wa Bujumbura tena idadi kubwa ya hao wakiwa wanatoka kwenye familia maskini sana ambazo zinategemea matunda ya shamba zao ili kuweza kula au kujisogeza kwa jambo  lolote.`Résultat de recherche d'images pour "université du burundi"
Kwa asilimia kubwa inaonekana kwamba Chuo kikuu cha Burundi na Chuo Kikuu cha Ualimu(ENS) ndivyo vinawapokea watoto kutoka familia ndogo.
Watoto hao ambao walikuwa wameshazoea maisha ya kijijini huashiri matatizo mengi kutokana na ughali wa bidhaa sokoni huku famila zao zikiwa hazina uwezo wa kutimiza maitaji ya watoto wao.
Wanapofika mjini Bujumbura, vijana hao huchaguwa kuishi katika kata ndogondogo ambazo zinawaruhusu kuishi japo kidogo kutokana na uwezo wao. Kata hizo ni : Kamenge hasa kwa wanaosoma kwenye Chuo kikuu cha Ualimu(ENS), na Mugoboka na Kanyari kwa wanaosomakwenye chuo kikuu cha Burundi.
Tunapoachana kidogo na hao ambayo wanachuo wanakutana nayo kwenye vitongoji mbalimbali, kuna pia wanaoishi kwenye mabewa tofauti ambazo zina uwezo wa kuwalaza.Na wao pia huishi maisha tofauti : kuna ambao wanaruhusiwa kulala na pia wakalishwa na wanaolala bila kulishwa.
Kawaida mwanafunzi aliyebahatika kufaulu mtihani wa kufuzu masomo ya chuo kikuu alikuwa anapokea Ruzuku ya kumusaidia kupambana japo kidogo na maisha magumu ya mjini Bujumbura. Akiwa anasoma mwanachuo huitaji mambo mengi kama kula, itaji ambalo ni lazima,kucapisha au kununuwa karatasi, sabuni na vingine vifa ambavyo ni muhimu kwa kuendeleza maisha ya mwanachuo.
Kutokana na mfumo mpya wa serikali ya Burundi ya kumpa kila mwanachuo ruzuku ya kulipwa inayokaribia elfu miya moja na themanini kila miezi mitatu, maisha ya mwanachuo yalikuwa yameanza kuonesha unafu, ila kutokana na kuvhelewa kwa pesa hizo, ruzuku hiyo inawakuta tayari wameshaingia kwenye mikopo.
Kwa mfano mwaka huu 2019, wanafunzi hao ambao wanapewa ruzuku ya kulipwa wamejikuta kwenye sitofahamu wa umaskini  usiyoeleweka hasa hasa wale wanaoishi katika kata za Kanyari na Mugoboka kwa sababu walilazimika kusubiri miezi isiyopungua tatu ili kuweza kunasa pesa hizo.
Baadhi ya wanachuo walishindwa kuvumilia na kurudi vijijini kwao huku wakiwa wameshaingia kwenye matatizo na wanaopangisha nyumba kwa kushinda kulipa pesa kwa mda ambao walikuwa wameahidiana.
Kwa kweli, ugumu wa maisha ya mwanachuo unaeleweka kwa wazi unapochambuwa vizuli na kuweza kufananisha na yale aliokuwa anaishi mwanachuo wa miaka ile ya nyuma.kila siku bei ya vitu sokoni inapanda wakati mapato yamebaki ni yaleyale, ina maana kwamba ruzuku ruzuku bado haijaongezeka.
Mwanachuo enzi zile alikuwa anapata zaidi ya elfu thelethini na bei ya bidhaa sokoni ilikuwa nzuri sana mpaka mwanachuo anayeishi kwenye nyumba ya kupanga alikuwa anabakiza karibu nusu ya ruzuku, kumanisha kwamba aliweza hata kununua nguo nzuri na kupata kinywaji fulani. Tofauti na sasa ambapo mambo yamekwenda kombo.Licha ya ruzuku kupunguzwa(kutoka  elfu 31000 kwenda elfu 28000), kil akitu kila kitu sokoni kimepanda bei mala zaidi ya tano . Na hivyo kufanya mwanachuo kuonja ugumu wa maisha ya mji mkuu.
Ili kutimiza maitaji ya mwanachuo, sanasana wale wanaoishi kwenye kata mbalimbali, hulazimika kuongeza kitita fulani vha pesakwa ile ruzuku wanaopewa wakati familia zao zinaumbwa na matatizo kule vijijini ikiwemwo ikiwemwo kuwalipia ada wale wadogo waliobaki kule.
Kama ilivyowahi kusema hapo juu, wanaoishi kwenye nyumba za vyuo nao maisha yao huwa mabaya muda mwingine : ukitazama chakula wanachopewa unakuta wanabaniwa na hivyo hubaki na njaa. Hiyo ni tatizo kubwa kwa sababu huwezi kusoma na kuelew vizuli wakati tumboni mambo sio mazuri.
Kwa upande wa wanaoishi kule bila bila cheti kinachowaluhusu kula nao hukutana na matatizo mengi kwa sababu wanalazimika kwenda kununua chakula kidogo  kwa bei isiyo chini ya miya saba(700fbu).
Siwezi pia kusahau wenzangu wanaosoma kwenye vyuo vya watu binafsi. Mtu fulani angeweza kusema kwamba wao wanaishi vizuli kwa kufikilia kwamba wao wana familia kubwa ambazo ziko tayari kuwanunulia kila kitu. Ila unapojaribu kuongea na wanaposoma kule wanakuelezea vizuri kwamba si wote  ambao wanaishi maisha ya kusifia.
Mzazi au mtu mwingine anapokupa ahadi ya kukulipia masomo unakuta mwisho wa siku vile vifaa vidogovidogo mwanachuo anajinunulia mwenyewe kama vile karatasi, sabuni, nguo na vyinginevyo.kuna pia wanaotengwa na kuachwa njipandana wale ambao walikuwa wamewanyemelea kuwalipia na kuwajali kwa kila jambo.
Vile vile, kama nilivyowahi kusema, wanachuo wanaopanga kule kwenye kata ndogondogo, wakidhania kwamba maisha kule yatakuwa rahisi ,hukuta mambo kinyume kwa vile walikuwa wanategemea. Unakuta wanafunzi sita au zaidi wanaishi pamoja kwenye nyumba ndogo sana . kutokana na joto kali, hawawezi kudurusu kwa urahisi na hivyo kuwafanya kutotimiza vizuri lengo lao la kwanza ambalo ni kusoma. Kwani kusoma kunaitaji mwingi na utulivu kichwani pia nao unatakiwa ila wanajishughurisha kwa kupika, kwenda kuchota maji na kutafuta bidhaa sokoni.
Kama kweli mwanachuo ndiwo kiongozi wa kesho, ndiwo atakayekuwa mwalimu siku zijazo, kwa ujumla kama ndiye atakayeyitunza na kuyisogeza mbele nchi yetu ya Burundi ; kwa nini serikali isijaribu hata kidogo kuyafanya maisha ya mwanachuo yawe mazuri ili aweze kusoma akiwa kwenye hali ya utulivu bila mambo ya kumuchokesha kichwa nje ya masomo ?
Kama unataka mti wako ulete matunda kesho, kwa nini usiutunze leo ukiwa bado mdogo ?
Kwa muono wangu mimi, serikali  ingejaribu kuwakusanya wanachuo na kuwaweka kwenye nyumba za chuo ili kuhakikisha au wajaribu kuwapatia kwa muda mzuri ruzuku wale wanaopanga kwenye kata mbalimbali ili kuhakikisha maisha yao wanayafuata kwa ukaribu kwa sababu ni vigumu kusoma huku ukiwa na presha kichwani kwa kufikiria nitakula nini au nitamlipa nini bosi wangu.
Tena viongozi wa vyuo vyote wangewezwa kujitahidi na kutumia nguvu ili wajue maisha ya mwanachuo kule kwenye kata au vitongoji (Kanyari, Mugoboka, Kamenge,…) yanaendeleaje.  Na hayo yangeweza kuwasaidia kutunga ripoti nzuri ya kuwajulisha serikalini wajuwe kipi cha kufanya ili maisha ya mwanachuo yabadirike na yawe yakutamania
Résultat de recherche d'images pour "université du burundi"


 Par IRAKOZE Innocent