Katika nchi
yetu ya Burundi, kama ilivyo katika nchi nyingine, kuna wingi wa vyuo. Ukitoa
Chuo kikuu Cha Burundi na chuo kikuu cha Ualimu ENS ambavyo ni vya serikali,
kuna pia vyua vyingi ambavyo ni vya watu binafsi. Na hivyo mtu hulipa ili aweze
kupata masomo ya vyuo hivyo.
Kila mwaka,
vyuo hivyo(vya kiserikali na visivyo vya kiserikali)huwaleta wanafunzi kutoka
shule mbalimbali za sekondali nchini kote.Ndiyo maana ningependa niyazungumuzie
kwa ufasaa maisha ya mwanachuo mjini Bujumbura.
Vyuo
vinawapokea wanafunzi wengi.baadhi ya hao wanatoka vijijini mbali na mji wa
Bujumbura tena idadi kubwa ya hao wakiwa wanatoka kwenye familia maskini sana
ambazo zinategemea matunda ya shamba zao ili kuweza kula au kujisogeza kwa
jambo lolote.`
Kwa asilimia
kubwa inaonekana kwamba Chuo kikuu cha Burundi na Chuo Kikuu cha Ualimu(ENS)
ndivyo vinawapokea watoto kutoka familia ndogo.
Watoto hao
ambao walikuwa wameshazoea maisha ya kijijini huashiri matatizo mengi kutokana
na ughali wa bidhaa sokoni huku famila zao zikiwa hazina uwezo wa kutimiza
maitaji ya watoto wao.
Wanapofika
mjini Bujumbura, vijana hao huchaguwa kuishi katika kata ndogondogo ambazo
zinawaruhusu kuishi japo kidogo kutokana na uwezo wao. Kata hizo ni :
Kamenge hasa kwa wanaosoma kwenye Chuo kikuu cha Ualimu(ENS), na Mugoboka na
Kanyari kwa wanaosomakwenye chuo kikuu cha Burundi.
Tunapoachana
kidogo na hao ambayo wanachuo wanakutana nayo kwenye vitongoji mbalimbali, kuna
pia wanaoishi kwenye mabewa tofauti ambazo zina uwezo wa kuwalaza.Na wao pia
huishi maisha tofauti : kuna ambao wanaruhusiwa kulala na pia wakalishwa
na wanaolala bila kulishwa.
Kawaida
mwanafunzi aliyebahatika kufaulu mtihani wa kufuzu masomo ya chuo kikuu alikuwa
anapokea Ruzuku ya kumusaidia kupambana japo kidogo na maisha magumu ya mjini
Bujumbura. Akiwa anasoma mwanachuo huitaji mambo mengi kama kula, itaji ambalo
ni lazima,kucapisha au kununuwa karatasi, sabuni na vingine vifa ambavyo ni
muhimu kwa kuendeleza maisha ya mwanachuo.
Kutokana na
mfumo mpya wa serikali ya Burundi ya kumpa kila mwanachuo ruzuku ya kulipwa
inayokaribia elfu miya moja na themanini kila miezi mitatu, maisha ya mwanachuo
yalikuwa yameanza kuonesha unafu, ila kutokana na kuvhelewa kwa pesa hizo,
ruzuku hiyo inawakuta tayari wameshaingia kwenye mikopo.
Kwa mfano
mwaka huu 2019, wanafunzi hao ambao wanapewa ruzuku ya kulipwa wamejikuta
kwenye sitofahamu wa umaskini
usiyoeleweka hasa hasa wale wanaoishi katika kata za Kanyari na Mugoboka
kwa sababu walilazimika kusubiri miezi isiyopungua tatu ili kuweza kunasa pesa
hizo.
Baadhi ya
wanachuo walishindwa kuvumilia na kurudi vijijini kwao huku wakiwa wameshaingia
kwenye matatizo na wanaopangisha nyumba kwa kushinda kulipa pesa kwa mda ambao
walikuwa wameahidiana.
Kwa kweli,
ugumu wa maisha ya mwanachuo unaeleweka kwa wazi unapochambuwa vizuli na kuweza
kufananisha na yale aliokuwa anaishi mwanachuo wa miaka ile ya nyuma.kila siku
bei ya vitu sokoni inapanda wakati mapato yamebaki ni yaleyale, ina maana
kwamba ruzuku ruzuku bado haijaongezeka.
Mwanachuo
enzi zile alikuwa anapata zaidi ya elfu thelethini na bei ya bidhaa sokoni
ilikuwa nzuri sana mpaka mwanachuo anayeishi kwenye nyumba ya kupanga alikuwa
anabakiza karibu nusu ya ruzuku, kumanisha kwamba aliweza hata kununua nguo
nzuri na kupata kinywaji fulani. Tofauti na sasa ambapo mambo yamekwenda
kombo.Licha ya ruzuku kupunguzwa(kutoka
elfu 31000 kwenda elfu 28000), kil akitu kila kitu sokoni kimepanda bei
mala zaidi ya tano . Na hivyo kufanya mwanachuo kuonja ugumu wa maisha ya mji
mkuu.
Ili kutimiza
maitaji ya mwanachuo, sanasana wale wanaoishi kwenye kata mbalimbali,
hulazimika kuongeza kitita fulani vha pesakwa ile ruzuku wanaopewa wakati
familia zao zinaumbwa na matatizo kule vijijini ikiwemwo ikiwemwo kuwalipia ada
wale wadogo waliobaki kule.
Kama
ilivyowahi kusema hapo juu, wanaoishi kwenye nyumba za vyuo nao maisha yao huwa
mabaya muda mwingine : ukitazama chakula wanachopewa unakuta wanabaniwa na
hivyo hubaki na njaa. Hiyo ni tatizo kubwa kwa sababu huwezi kusoma na kuelew
vizuli wakati tumboni mambo sio mazuri.
Kwa upande wa
wanaoishi kule bila bila cheti kinachowaluhusu kula nao hukutana na matatizo
mengi kwa sababu wanalazimika kwenda kununua chakula kidogo kwa bei isiyo chini ya miya saba(700fbu).
Siwezi pia
kusahau wenzangu wanaosoma kwenye vyuo vya watu binafsi. Mtu fulani angeweza
kusema kwamba wao wanaishi vizuli kwa kufikilia kwamba wao wana familia kubwa
ambazo ziko tayari kuwanunulia kila kitu. Ila unapojaribu kuongea na wanaposoma
kule wanakuelezea vizuri kwamba si wote
ambao wanaishi maisha ya kusifia.
Mzazi au mtu
mwingine anapokupa ahadi ya kukulipia masomo unakuta mwisho wa siku vile vifaa
vidogovidogo mwanachuo anajinunulia mwenyewe kama vile karatasi, sabuni, nguo
na vyinginevyo.kuna pia wanaotengwa na kuachwa njipandana wale ambao walikuwa
wamewanyemelea kuwalipia na kuwajali kwa kila jambo.
Vile vile,
kama nilivyowahi kusema, wanachuo wanaopanga kule kwenye kata ndogondogo,
wakidhania kwamba maisha kule yatakuwa rahisi ,hukuta mambo kinyume kwa vile
walikuwa wanategemea. Unakuta wanafunzi sita au zaidi wanaishi pamoja kwenye
nyumba ndogo sana . kutokana na joto kali, hawawezi kudurusu kwa urahisi na
hivyo kuwafanya kutotimiza vizuri lengo lao la kwanza ambalo ni kusoma. Kwani
kusoma kunaitaji mwingi na utulivu kichwani pia nao unatakiwa ila wanajishughurisha
kwa kupika, kwenda kuchota maji na kutafuta bidhaa sokoni.
Kama kweli
mwanachuo ndiwo kiongozi wa kesho, ndiwo atakayekuwa mwalimu siku zijazo, kwa
ujumla kama ndiye atakayeyitunza na kuyisogeza mbele nchi yetu ya
Burundi ; kwa nini serikali isijaribu hata kidogo kuyafanya maisha ya
mwanachuo yawe mazuri ili aweze kusoma akiwa kwenye hali ya utulivu bila mambo
ya kumuchokesha kichwa nje ya masomo ?
Kama unataka
mti wako ulete matunda kesho, kwa nini usiutunze leo ukiwa bado mdogo ?
Kwa muono wangu
mimi, serikali ingejaribu kuwakusanya
wanachuo na kuwaweka kwenye nyumba za chuo ili kuhakikisha au wajaribu
kuwapatia kwa muda mzuri ruzuku wale wanaopanga kwenye kata mbalimbali ili
kuhakikisha maisha yao wanayafuata kwa ukaribu kwa sababu ni vigumu kusoma huku
ukiwa na presha kichwani kwa kufikiria nitakula nini au nitamlipa nini bosi
wangu.
Tena viongozi
wa vyuo vyote wangewezwa kujitahidi na kutumia nguvu ili wajue maisha ya
mwanachuo kule kwenye kata au vitongoji (Kanyari, Mugoboka, Kamenge,…) yanaendeleaje. Na hayo yangeweza kuwasaidia kutunga ripoti
nzuri ya kuwajulisha serikalini wajuwe kipi cha kufanya ili maisha ya mwanachuo
yabadirike na yawe yakutamania
Par IRAKOZE Innocent